Mtangazaji
wa Choice Fm, mwanamuziki, balozi wa vijana Tanzania, ameonyesha
kukasirishwa na kitendo cha Gazeti la Babukubwa kuweka picha tofauti na
walizokubaliana kwenye ukurasa wa mbele ambao ndio ukurasa wa mauzo wa
gazeti (front page)
Akizungumza na XXL vanessa amesema, picha iliyowekwa katika ukurasa wa
mbele, sio picha iliyotakiwa kuwepo hapo, walipiga picha nyingi sana
wakati wa session ya photo shoot, na kukubaliana picha zinazofaa kutoka
lakini matokeo yake wametoa tofauti na makubaliano.
"Tulikuwa tumeshachagua picha za front page na zile zitakazotokea ndani, za front page zilikuwa na version mbili na hakuna hata moja waliyoitoa, hata ukiangalia the headline, Ommy dimpoz ampata Vanessa, ukisoma tu unaelewa nini? ingawa story ni tofauti ndani lakini wangapi wanaliona gazeti na wananua kusoma kilichoandikwa ndani? aliuliza Vanessa.
"It is
so disrespectful, wanaharibu reputation, because my brand doesn't stand
for that, wanaweza kukukosesha opportunities in the future."
No comments:
Post a Comment