Jamaa kasafiri kikazi kwenda mkoani akamuacha mpenzi wake Dar maeneo ya Mabibo.
Jamaa
kasafiri kikazi kwenda mkoani akamuacha mpenzi wake Dar maeneo ya
Mabibo. Baada ya kama miezi miwili hivi binti akamuandikia jamaa barua:
"Bakari naona mimi na wewe mapenzi yetu yamefika mwisho. Kwa miezi
miwili iliyopita nimeamua kuendelea na maisha yangu na tayari nishatoka
na Beda muuza chipsi na Kalimari muuza mchele wa jumla., la msingi isiwe
ugomvi, siwezi kuwa na mwanaume kama wewe usiye na mbele wala nyuma,
naomba tu nitumie ile picha yangu kila mtu achape mwendo kivyake." Jamaa
baada ya kuisoma roho ikamuuma sana. Akazunguka kwenye studio mbili
tatu za picha akapata picha kama za wasichana 19 hivi tofauti tofauti
halafu akaongeza na ya yule binti akamtumia kwa barua na ujumbe huu."Ki
ukweli bado sijaelewa wewe ni Jamila yupi. Nimewahi kuwa na wapenzi
wenye jina Jamila kama 20 hivi. Naomba uangalie picha yako ni ipi kati
ya hizo, ichukue then zinazobaki nitumie. Goodbye!"
No comments:
Post a Comment