Bw
Mohammed, mkazi wa Kigamboni jijini Dar amedaiwa kuwafanyia unyama
watoto wawili, akimlawiti mwanaye wa kufikia na kumbaka mdogo wa
mkewe.Akizungumza na mtandao huu juzi nyumbani kwake, mke wa mtuhumiwa
huyo, Zubeda alisema watoto waliofanyiwa hivyo ni mwanaye wa kiume (6)
na mdogo wake wa kike (16) (majina tunayo).
Mwanamke huyo
alisema: Nilikutana na Mohammed nikiwa na mtoto huyo wa kiume, ndani ya
uhusiano wetu tukajaliwa kupata mtoto wa kiume hivi karibuni, hapo
ndipo matatizo yalipoanza.
“Alihama chumba ili mimi nilale na
kichanga, akaenda kulala na mtoto huyo. Niliamini angemchukulia kama
mwanaye kwa kuwa tulishaoana.
“Mwaka jana alikuja mdogo wangu, tukabadili
kulala, tuliwaacha watoto hao walale chumba kimoja mume wangu akarudi
chumbani. Alizua tabia ya kutoka usiku eti kuvuta sigara kumbe alikuwa
anakwenda kumwingilia mdogo wangu,” alizidi kudai mwanamke huyo.
Alidai kuwa ikafika wakati akagundua
mwanaye huyo anajisaidia kwenye nguo na kinyesi kinakuwa na damu, akawa
anampiga na kumwamuru afue nguo mwenyewe.
“Nilimuuliza mtoto wangu ambapo aliniambia ni kweli baba yake amekuwa akienda chumbani kwao na kumfanyia mchezo mbaya.
“Ukweli taarifa hizo zilinishtua sana, sikutarajia mdogo wangu kama angeweza kulala na mume wangu, nilimpiga sana.
“Wakati namwadhibu mtoto wangu naye akaona
kumbe kitendo kile ni kibaya akasema hata yeye baba yake amekuwa
akimfanyia mchezo mchafu kila siku usiku,” alisema mama huyo huku
akilia.
Wakati watoto hao wakikiri kufanyiwa hivyo,
Mohammed alikuwa akiwasikia na kujitetea kwamba walikuwa wakimsingizia,
ghafla alipokea simu na kusema anakwenda kwenye biashara akirudi
watazungumzia suala hilo lakini hakurudi tena mpaka habari hii
inapoandikwa.
Baada ya kuona hivyo, mke huyo alikwenda
kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Kigamboni na kufungua kesi
mbili zenye namba KGD/RB/5218/2013 KUBAKA na KGD/RB/5244/2013 KULAWITI,
mpaka sasa mtuhumiwa huyo anasakwa na polisi.
Mwanamke huyo alisema alipewa PF3 na
kuwapeleka waathirika hao Hospitali ya Vijibweni na vipimo vilionesha
waliharibiwa sehemu zao za siri.
Mama huyo alisema daktari amemwambia mtoto wake wa kiume angeweza kupoteza uhai kama
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mji Mwema, Mwinyi Baishe alithibitisha kusikia madai hayo.
angeendelea kufanyiwa mchezo huo.
source:audifacejacksonblogspot
No comments:
Post a Comment