Usajili wa wachezaji mbalimbali unazidi kushika kasi barani ulaya.
Winga Mshambuliaji wa Ivory Coast, Gervais Lombe Yao Kouassi maarufu
kama Gervinho amekamilisha uhamisho wa kuichezea As Roma ya Italia.
Msimu wake wa kwanza aliifungia Arsenal magoli manne kabla ya kufunga magoli saba msimu uliopita.
Amekuwa akipata ushindani wa kuwemo kwenye kikosi cha kwanza cha
Arsene Wenger, na huenda usajili wake wa kuhamia Seria A utakuwa
changamoto mpya kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.
No comments:
Post a Comment