-NI RPC WA MKOA WA TEMEKE
Na Makongoro Oging'
NI jambo la kufurahisha kuona kwamba polisi wamekataa rushwa ya shilingi milioni 30 baada ya kuwakamata majambazi waliokuwa wakipakia sukari ya wizi jijini Dar es Salaam.
NI jambo la kufurahisha kuona kwamba polisi wamekataa rushwa ya shilingi milioni 30 baada ya kuwakamata majambazi waliokuwa wakipakia sukari ya wizi jijini Dar es Salaam.
Tukio
hilo lilitokea Jumapili iliyopita baada ya polisi kukamata magunia 1,312
ya sukari yenye thamani ya shilingi milioni 90.5 yaliyoibwa katika
ghala la kuhifadhia bidhaa la Haruni Zacharia Enterprises lililopo
Mbagala, wilayani Temeke, Dar.
Polisi
hao ambao wako chini ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, ACP
Engelbert Kiondo imeelezwa na chanzo chetu kuwa walikataa rushwa hiyo
baada ya kuwakamata majambazi 12 wenye silaha za moto na mapanga baada
ya kuwakuta laivu wakipakia mifuko ya sukari katika lori la kubebea
mizigo.
Akithibitisha habari hiyo, Kamanda Kiondo alisema ni kweli tukio hilo lilitokea siku hiyo.
“Ilikuwa ni saa mbili usiku ambapo walinzi wanne waliokuwa wakilinda ghala hilo walivamiwa na kufungwa kamba kisha kujeruhiwa kwa mapanga na majambazi kuvunja geti na kuingiza lori, wakapakia sukari,” alisema Kiondo.
Aliongeza
kuwa jeshi lake lilifanikiwa kuyanasa majambazi hayo baada ya kupata
taarifa kutoka kwa raia wema na baada ya kuwakamata walitaka kutoa
rushwa ya shilingi milioni 30 ili waachiwe lakini vijana wake walikataa
na kuwafikisha kituoni.
“Nawataka
majambazi wote waache shughuli hiyo kwani msako mkali umeanza dhidi yao
na nawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa polisi kwa
kuwafichua wahalifu wote ili tuishi kwa amani’,”alisema kamanda
huyo.CHANZO:GLOBAL PUBLISHER BLOG
No comments:
Post a Comment