Saturday, August 31, 2013

Aliyoyasema Edward Lowassa kuhusu President Kikwete Washington DC.

.
.
Swahili TV wa swahilitv.blogspot.com ambao wanafanya kazi zao wakiwa Washington DC Marekani, walikutana na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Edward Lowassa kwenye mji huo na kufanya nae interview.
Moja ya alivyovisema Mbunge huyu wa Monduli kuhusu President Kikwete, ni kumsifia kwamba kaifanya Tanzania kupata heshima kimataifa.
 
Anasema kitendo cha Rais wa Marekani Barack Obama kuitembelea Tanzania pamoja na
viongozi mbalimbali wa mataifa makubwakumeonyesha Rais Kikweteanakubalika.
Amekaririwa akisema ‘Ni hivi karibuni  tu  Rais Xi Jinping wa China, Rais Obama na Rais mstaafu wa Marekani  George W.Bush walikuwa Tanzania, hii inaonyesha Tanzania iko juu katika kimataifa, Rais  Kikwete anastahili pongezi sana kwa hilo kwani sio rahisi kwa viongozi wa mataifa makubwa kutembelea nchi nyingine labda kama mko juu sana kimataifa’
Millardayo.com

No comments:

Post a Comment