Swahili TV wa
swahilitv.blogspot.com ambao wanafanya kazi zao wakiwa Washington DC
Marekani, walikutana na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Edward Lowassa kwenye mji huo na kufanya nae interview.
Moja ya alivyovisema Mbunge huyu wa Monduli kuhusu President Kikwete, ni kumsifia kwamba kaifanya Tanzania kupata heshima kimataifa.
Anasema kitendo cha Rais wa Marekani Barack Obama kuitembelea Tanzania pamoja na
viongozi mbalimbali wa mataifa makubwakumeonyesha Rais Kikweteanakubalika.
Amekaririwa akisema ‘Ni hivi karibuni tu Rais Xi Jinping wa China, Rais Obama na Rais mstaafu wa Marekani George W.Bush walikuwa Tanzania, hii inaonyesha Tanzania iko juu katika kimataifa, Rais
Kikwete anastahili pongezi sana kwa hilo kwani sio rahisi kwa viongozi
wa mataifa makubwa kutembelea nchi nyingine labda kama mko juu sana
kimataifa’
Millardayo.com