Watu wengi
walitegemea kuiona picha ya kwanza ya mtoto North West hapo jana lakini
mambo yalikwenda ndivyo sivyo. Haitaweza kutokea. Ripoti ya karibuni
inafichua kuwa Kanye West na Kim Kardashian wamekataa ofa za mamilioni
ya dola za kimarekani zilizotoka kila pande kwaajili ya kuuza picha ya
mtoto wao.
Wenyewe Kanye na Kim wanasema mtoto wao hauziki kwa pesa yoyote ile.
Tangu Kim alipojifungua mapema kuliko ilivyotarajiwa Juni 15, ofa
kubwa iliyotolewa kwa wazazi hao wenye kujiskia ilitoka kwa jarida moja
la Australia wakiwa wameweka mezani dola milioni 3. Lakini kiasi hicho
hakikutosha na hakuna kiasi kitakachotosha.
Ripoti za awali zilisema kwamba kama wazazi hao waataamua kuuza picha
ya kwanza ya mtoto wao, basi pesa zote zitakwenda kusaidia mambo ya
kijamii.
Lakini mpaka muda huu inaonekana kama vile na wao wameamua kufuata
nyayo za Beyoncé na Jay-Z, ambao walizuia picha za mtoto wao Blue Ivy
Carter kwa karibu mwaka mzima
No comments:
Post a Comment